Tuesday, January 24, 2012

ALLY REHMTULLAH ATISHA KATIKA UBUNIFU WA MAVAZI


Ubunifu wa mavazi ni miongoni mwa fani inayozidi kukua siku hadi siku duniani pote kutokana na maendeleo katika uvaaji wa mitindo mbali mbali kulingana na eneo na tukio.

Ally Aurora.com liliweza kupata nafasi ya kumtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Ally Rehmtullah na kuzungumza nae machache na kuelezea alipoanzia na matarajio yake ya baadae katika fani hiyo ya mitindo.
Anaanza kwa kusema “Ili ufanikiwe katika suala la ubunifu wa mitindo unahitaji kulifahamu vizuri umbo la kike, mitindo na mavazi ya wanawake ambayo ndiyo inakupa changamoto mbunifu wa mitindo kufikiria na kubuni mitindo mipya ambayo inawavutia wanawake wengi zaidi ili wanunue nguo zao,” anasema Ally Rehmtullah.

Kijana huyu ambaye ni Mtanzania mwenye asili ya kihindi alilejea nchini mwaka 2006, baada ya kuhitimu shahada yake ya ubunifu wa mitindo katika chuo cha Lehigh, Pessivania nchini Marekani na kushiriki katika onyesho la Lady in Red lililoandaliwa na Asia Idarus asia Idarous lililofanyika January 2007.



Onyesho hilo lilimfanya Ally akatambulika na kuoneka kama mbunifu chipukizia ila si kama alivyo kwa sasa ambapo ukitamka jina lake hakuna aiyemfahamu.

Mbunifu huyu kwa tabia ni mcheshi na hupenda kubadirisha mawazo na watu mbali mbali na pia malengo yake makubwa ni kufanya kazi kwa bidii.

Mpaka sasa ameweza kufanya maonyesho mbali mbali likiwemo la Red in Red, Prison Break, Temptation, Delectables, Swahili Fashion Week, Rafda pamoja na nchi jirani ya Rwanda na Uganda ikiwemo na nchini Marekani.
“Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kunisaidia popote ninapokwenda huwa nakubalika na watu wanayapenda mavazi yangu,” anasema Ally Rehmtullah.

Alianza kuwika mwaka Oktoba 2006, pale alipobuni vazi la warembo walioshiriki wa miss Tanzania.
Akielezea matatizo wanayokumbana nayo anasema, “Tatizo kubwa linalotuangusha ni suala la ukosefu wa viwanda vya kutengeneza vitambaa,”.
“Ningeiomba serikali itafute wawekezaji waweze kuwekeza kwenye suala la viwanda vya kutengeneza vitambaa ili kutupunguzia gharama nadhani hata nguo tunazobuni na kushona tutaziuza kwa bei nafuu,” anasema Ally.

Pia suala lingine linalowaangusha katika maonyesho yao ni kukosa wadhamini ambao watatufanya kazi tunatoifanya isogee mbele kuliko kutumia hela ndogo tulizo nazo,” anasema.

Nilipomuuliza ni kitu gani alijifunza alipokuwa kwenye maonyesho yalifanyika nchini Marekani,” anasema “Kiukweli wenzetu wameelimika sana hasa kwenye suala la ubunifu wa mavazi maana hauwezi kuleta mavazi yao huku kwa kuwa utamaduni wa nchi yetu ni tofauti na wa nchi yetu,”

Akielezea matatizo wanayokumbana nayo anasema, “Tatizo kubwa linalotuangusha ni suala la ukosefu wa viwanda vya kutengeneza vitambaa,”.
“Ningeiomba serikali itafute wawekezaji waweze kuwekeza kwenye suala la viwanda vya kutengeneza vitambaa ili kutupunguzia gharama nadhani hata nguo tunazobuni na kushona tutaziuza kwa bei nafuu,” anasema Ally.
Aliongezea kuwa, “Wao wanamavazi mazuri ila kwenye suala la heshima hakuna katika kuvaa, mtu anaweza kuvaa kinguo cha ovyo ambacho kwa kweli kwetu unaweza kupigwa mawe na kuzomewa,”

Pia alisema kuwa anakumbuka alipokuwa amekwenda Zanzibar kufanya fashion show alipata changamoto kidogo “Kuna baadhi ya nguo walipokagua hawakutaka nizifanyie onyesho maana viongozi hao walisema haziendani na tamaduni zao,”.

Kijana huyu anayependelea kuvaa Jean na T-shirt anasema, “Anasema anamshukuru sana wanamitindo wenzake kwa kumpa sapoti ya kutosha katika kazi zake.

Nilipomuuliza suala la soko lao, anasema “Soko la bidhaa zetu lipo hapa hapa nchini na huwa tunalitangaza kwa kufanya fashion show mbali mbali.