Ubunifu wa mavazi ni miongoni
mwa fani inayozidi kukua siku hadi siku duniani pote kutokana na maendeleo
katika uvaaji wa mitindo mbali mbali kulingana na eneo na tukio.
Ally Aurora.com liliweza kupata
nafasi ya kumtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam, Ally Rehmtullah na
kuzungumza nae machache na kuelezea alipoanzia na matarajio yake ya baadae
katika fani hiyo ya mitindo.
Anaanza kwa kusema “Ili
ufanikiwe katika suala la ubunifu wa mitindo unahitaji kulifahamu vizuri umbo la
kike, mitindo na mavazi ya wanawake ambayo ndiyo inakupa changamoto mbunifu wa
mitindo kufikiria na kubuni mitindo mipya ambayo inawavutia wanawake wengi zaidi
ili wanunue nguo zao,” anasema Ally Rehmtullah.
Kijana huyu ambaye ni Mtanzania
mwenye asili ya kihindi alilejea nchini mwaka 2006, baada ya kuhitimu shahada
yake ya ubunifu wa mitindo katika chuo cha Lehigh, Pessivania nchini Marekani na
kushiriki katika onyesho la Lady in Red lililoandaliwa na Asia Idarus asia
Idarous lililofanyika January 2007.
Onyesho hilo lilimfanya Ally
akatambulika na kuoneka kama mbunifu chipukizia ila si kama alivyo kwa sasa
ambapo ukitamka jina lake hakuna aiyemfahamu.
Mbunifu huyu kwa tabia ni
mcheshi na hupenda kubadirisha mawazo na watu mbali mbali na pia malengo yake
makubwa ni kufanya kazi kwa bidii.
Mpaka sasa ameweza kufanya
maonyesho mbali mbali likiwemo la Red in Red, Prison Break, Temptation,
Delectables, Swahili Fashion Week, Rafda pamoja na nchi jirani ya Rwanda na
Uganda ikiwemo na nchini Marekani.
“Napenda kumshukuru Mwenyezi
Mungu kwa kuweza kunisaidia popote ninapokwenda huwa nakubalika na watu
wanayapenda mavazi yangu,” anasema Ally Rehmtullah.
Alianza kuwika mwaka Oktoba
2006, pale alipobuni vazi la warembo walioshiriki wa miss Tanzania.
Akielezea matatizo wanayokumbana nayo anasema, “Tatizo kubwa linalotuangusha
ni suala la ukosefu wa viwanda vya kutengeneza vitambaa,”.
“Ningeiomba serikali itafute
wawekezaji waweze kuwekeza kwenye suala la viwanda vya kutengeneza vitambaa ili
kutupunguzia gharama nadhani hata nguo tunazobuni na kushona tutaziuza kwa bei
nafuu,” anasema Ally.
Pia suala lingine
linalowaangusha katika maonyesho yao ni kukosa wadhamini ambao watatufanya kazi
tunatoifanya isogee mbele kuliko kutumia hela ndogo tulizo nazo,” anasema.
Nilipomuuliza ni kitu gani
alijifunza alipokuwa kwenye maonyesho yalifanyika nchini Marekani,” anasema
“Kiukweli wenzetu wameelimika sana hasa kwenye suala la ubunifu wa mavazi maana
hauwezi kuleta mavazi yao huku kwa kuwa utamaduni wa nchi yetu ni tofauti na wa
nchi yetu,”
Akielezea matatizo wanayokumbana nayo anasema, “Tatizo kubwa linalotuangusha
ni suala la ukosefu wa viwanda vya kutengeneza vitambaa,”.
“Ningeiomba serikali itafute
wawekezaji waweze kuwekeza kwenye suala la viwanda vya kutengeneza vitambaa ili
kutupunguzia gharama nadhani hata nguo tunazobuni na kushona tutaziuza kwa bei
nafuu,” anasema Ally.
Aliongezea kuwa, “Wao wanamavazi mazuri ila kwenye suala la heshima hakuna
katika kuvaa, mtu anaweza kuvaa kinguo cha ovyo ambacho kwa kweli kwetu unaweza
kupigwa mawe na kuzomewa,”
Pia alisema kuwa anakumbuka
alipokuwa amekwenda Zanzibar kufanya fashion show alipata changamoto kidogo
“Kuna baadhi ya nguo walipokagua hawakutaka nizifanyie onyesho maana viongozi
hao walisema haziendani na tamaduni zao,”.
Kijana huyu anayependelea kuvaa
Jean na T-shirt anasema, “Anasema anamshukuru sana wanamitindo wenzake kwa kumpa
sapoti ya kutosha katika kazi zake.
Nilipomuuliza suala la soko lao,
anasema “Soko la bidhaa zetu lipo hapa hapa nchini na huwa tunalitangaza kwa
kufanya fashion show mbali mbali.
No comments:
Post a Comment